Sunday, November 18, 2018

MAGONJWA YA MOYO



MAGONJWA YA MOYO

Utangulizi
  • Watu million 17.9 hufa kwa magonjwa ya moyo dunia nzima kila mwaka. Huu ni sawa na 31% ya vifo vyote duniani.
  • Zaidi ya 75% ya vifo hivi hutoka kwenye nchi zenye uchumi wa chini na wa kati.
  • 85% ya vifo vyote visababishwavyo na ugonjwa wa moyo husababishwa na mshtuko wa moyo au kiharusi.


Magonjwa ya moyo au cardiovascular diseases ni magonjwa ambayo hutokana na moyo kutofanya kazi vizuri au changamoto kwenye mishipa inayosafirisha damu. Magonjwa haya ni kama, coronary artery disease, changamoto ya  mmapigo ya moyo, kiharusi, maumivu ya kifua (angina) na changamoto za kuzaliwa nazo.

Changamoto nyingi zinazotokana na magonjwa ya moyo zinaweza kuzuiwa au kutatuliwa kwa kufanya mabadiliko kwenye mfumo wa maisha.


Dalili

Dalili za kuwa na magonjwa ya moyo ni;
  • Maumivu ya kifua.
  • Kuishiwa pumzi au kupumua kwa shida.
  • Maumivu, Ganzi, Ulegevu au Ubaridi kwenye miguu au mikono kama mishipa ya damu kwenye hivyo viungo imebana.
  • Maumivu kwenye shingo, taya, kootumbo la juu au mgongo.
  • Mapigo yasiyo na mpangilio maalum.
  • Kuvimba miguu.
  • Uchovu.
  • Kizunguzungu.

Inawezekana usijulikane kuwa una magonjwa ya moyo mpaka ukipata mshtuko wa moyo hivyo ni muhimu kuhakikisha unacheki hizi dalili za magonjwa ya moyo na ujadiliane na daktari wako kama una wasi wasi wa kuwa nayo.




Vitu vinavyoweza kusababisha magonjwa ya moyo
  • Umri. Umri huongeza hatari ya mishipa ya damu kuharibika au kusinyaa na misuli ya moyo kulegea au kutanuka.
  • Jinsia. Wanaume wana hatari kubwa ya kupata magonjwa ya moyo. Ingawa hatari huongezeka kwa wanawake baada ya kukoma hedhi. 
  • Historia ya familia. Historia ya familia ya magonjwa ya moyo huongeza hatari ya kupata magonjwa hayo haswa kama mzazi alipatwa ugonjwa mapema (umri wa miaka 55 kwa ndugu wa kiume, kama baba au kaka, na umri wa 65 kwa ndugu wa kike kama dada au mama). 
  • Uvutaji wa sigara. Nicotine inayopatikana kwenye sigara hufanya mishipa ya damu kuziba na carbon dioxide uharibu kuta za mishipa ya damu na kusababisha changamoto za magonjwa ya moyo. Wavuta sigara hupatwa na mishtuko ya moyo zaidi ya wasiovuta sigara. 
  • Tiba za mionzi kwa wagonjwa wa saratani. Baadhi ya dawa na tiba za mionzi za saratani zinaweza kuongeza hatari ya kupata magonjwa ya moyo. 
  •  Ulaji mbaya. Ulaji wa vyakula vyenye mafuta, sukari, chumvi na lehemu huchangia kwenye kukua kwa magonjwa ya moyo.
  • High blood pressure. Kiwango cha pressure ya damu kikiwa juu sana huweza kusababisha kutanuka kwa kuta za mishipa ya damu na kupunguza uwazi unaopitisha damu.
  • Kisukari. Kuwa na kisukari huongeza hatari ya kupata magonjwa ya moyo.
  • Uzito Uliokithiri. Uzito uliokithiri huongeza changamoto kwa kiasi kikubwa sana.
  • Msongo wa mawazo. Msongo wa mawazo husababisha uharibifu wa mishipa ya damu na kuoneza changamoto.


Kuzuia

Baadhi ya magonjwa ya moyo, kama hitilafu kwenye moyo, hayawezi kuzuilika. Bali unaweza ukazuia magonjwa mengi ya moyo kwa kubadili mfumo wako wa maisha. Mabadiliko hayo ni kama;

·         Kuacha uvutaji wa sigara na kukaa na wavutaji wa sigara.
·         Dhibiti magonjwa mengine kama kisukari, high blood pressure na lehemu.
·         Fanya mazoezi kwa dakika 30 kila siku kwa angalu siku 4 kwa wiki.
·         Kula vyakula visivyo na mafuta mengi na chumvi.
·         Kuwa na uzito sahihi.
·         Punguza msongo wa mawazo.



Tiba

Magonjwa ya moyo yana matibabu tofauti kutokana na changamoto yenyewe. Kwa mfano, kama changamoto ni maambukizi (infection) basi antibiotics zitatumika kuweza kutibu. Kwa ujumla, magonjwa ya moyo hutibiwa kwa hizi njia zifuatazo;
  • Mabadiliko ya tabia. Hii ni pamoja na kula vyakula vyenye mafuta kidogo na chumvi kidogo, kufanya mazoezi angalu kwa dakika 30 kwa siku angalau mara 4 kwa wiki,kuacha uvutaji wa sigara na kunywa pombe kwa kiasi. 
  • Dawa. Kama mabadiliko ya tabia hayatoshelezi, daktari wako atakuandikia dawa kuweza kuratibu ugonjwa wa moyo. Aina ya dawa itatokana na ugonjwa wenyewe. 
  • Upasuaji. Kama dawa nazo hazitoshelezi, daktari wako atashauri upasuaji mdogo/mkubwa ili kurekebisha tatizo.



Hitimisho

Magonjwa mengi ya moyo yanaweza kuhepukika na kurekebishwa kwa kubadilisha mfumo wa maisha. Kwa kupunguza uzito na kufikia uzito sahihi kutokana na urefu wako. Punguzo la kilo 5 linaweza kusaidia kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa ya moyo na mengine yasiyoambukizwa kwa asilimia kubwa. Pia kula milo iliyokamilika isiyokuwa na mafuta mengi na chumvi nyingi. Mazoezi pia husaidia kwenye kuhakikisha moyo unafanya kazi vizuri lakini pia kwenye kupunguza uzito.

Kwa ujumla, unaweza kurekebisha afya yako kwa kubadili mambo madogo madogo kwenye maisha yako.

Kwa maswali zaidi na ushauri wa jinsi unavyoweza kuyazingatia haya kwa njia rahisi wasiliana nasi kwa namba +255 755 518 289.

Karibu sana.





Saturday, November 17, 2018

VITAMINI NNE MUHIMU KWA KUBALANCE HORMONES KWA WANAWAKE




Vitamini 4 Muhimu kwa kubalance hormones kwa Wanawake.

Je ni vitamini zipi muhimu kwa ajili ya kuratibu hormones kwa wanawake? Kutokuwa na uwiano sahihi wa hormone ni chanzo cha changamoto nyingi za kiafya kwa wanawake.Wanawake hupitia mabadiliko mengi ya hormone kwenye maisha yao – wakati wa hedhi, PMS, ujauzito na wakati wa kukoma hedhi.
Mabadiliko haya ya hormone yanaweza kusababisha kula hovyo, kukosa nguvu, msongo wa mawazo, chunusi, na maumivu. Pia yanaweza kusababisha changamoto ya vimbe kwenye ovary au kwa lfha ya kitaalam, PCOS.
Sababu za “Hormonal Imbalance” kwa wanawake.
Kuna sbabu nyingi za “hormonal imbalances” kwa wanawake.
Kutokana na mchakato wa asili wa kuzeeka, kutoka kwenye hedhi mpaka kukoma hedhi, mabadiliko ya hormones hutokea.
Lakini, kuna mambo mengine kwenye mazingira kama uchafuzi wa mazingira, vyakula vya viwandani, sumu kwenye bidhaa za usafi na urembo, nyama za viwandani pia hujulikana kwa kuvuruga uwiano wa hormone.
Vyakula navyo vina mchango mkubwa sana kwenye afya na uwiano wa hormones. Kula vyakula vingi vyenye sukari, mafuta, wanga, vihifadhi vya bandia (artificial preservatives), na kupuuzia ulaji wa vyakula vyenye vitamini, madini na viondosha sumu kama matunda, mboga mboga, mafuta mazuri, vyama za kienyeji (organic) na vyakula jamii ya karanga huunyima mwili virutubisho muhumi ambavyo hhuitajika kwa ajili ya kuweka uwiano sahihi wa hormones. Kwa sababu ni vigumu kupata virutubisho vyote muhimu kwa wingi unaohitajika kila siku, ni muhimu kutumia “Nutritional Supplements”.
Ingawa unahitaji kuwasiliana na daktari wako ili upate vipimo na matibabu sahihi ya “hormonal imbalance” na matatizo yanayohusiana nayo, unaweza ukaongeza ulaji wa vitamini hizi kwenye chakula chako. Hizi zitakusaidia kurekebisha tatizo la “Hormonal Imbalance” kwa njia asilia.

Sasa tunagalie vitamini muhimu kwa ajili ya “Hormonal Imbalances” kwa wanawake:

Vitamini 4 Muhimu kwa kubalance hormones kwa Wanawake.

1. Vitamini C
Vitamini C ni vitamini namba moja kwenye kuusaidia mwili kutengeneza hormone ya progesterone. Idadi kubwa ya wanawake wenye umri wa kuzidi miaka 35 hupata changamoto ya kuwa na upungufu wa hormone hii ya progesterone. Upungufu wa progesterone husababisha msongo wa mawazo, kukosa usingizi, na kuwa na wasiwasi.
·         Kiwango kinachohitajika: 75 – 100 mg kwa siku.
·         Matunda yana kiwango kizuri cha Vitamini C. Unaweza ukala machungwa, machenza, kiwi, strawberries na mananasi yana kiwango kizuri cha vitamini C.

2. Vitamini D
Wanawake wengi wana changamoto ya upungufu wa vitamini D ingawa ni vitamin muhimu sana. Upungufu wa vitamini D husababisha maumivu ya viungo, ukosefu wa nguvu, msongo wa mawazo, changamoto za tezi (thyroid).
·         Kiwango kinachohitajika: 400 – 800 IU kwa siku.
·         Vyanzo vizuri vya Vitamini D ni pamoja na dakika 20 za jua kila asubuhi, kiini cha yai, uyoga, na samaki.

3. Vitamini B-6
Moja kati ya vitamini muhimu kwenye “hormonal imbalance” kwa wanawake ni Vitamini B-6. Vitamini B-6 inasaidia kwa kupunguza dalili za PMS kwa wanawake kama moods, hasira, kusahau sahau, na tumbo kujaa gesi.
·         Kiwango kinachohitajika: 50 – 100 mg kwa siku.
·         Vyanzo vizuri vya Vitamini B-6 ni kama njegere, maini ya ng’ombe, samaki na kuku.

4. Vitamini E
Vitamini E ni kiondosha sumu kizuri sana. Ni muhimu kwa kila mwanamke ambaye anapitia ukomo wa hedhi maana hupata upungufu wa hormone ya “estrogen”. Kupata 50-400 IU kwa siku itasaidia kuratibu "hot flashes", ukavu kwenye uke, na "mood swings" ambavyo vyote hutokana na upungufu wa hormone ya estrogen.
·         Kiwango kinachohitajika: 22.4 IU kwa siku.
·         Vyanzo vizuri vya Vitamini E ni kama mafuta ya mimea,maharage, nafaka zisizo kobolewa, na almonds.

Matumizi ya Supplements
Kutokana na mabadiliko ya mazingira na njia za kulima mimea na matunda zilivyobadilika, ni rahisi kuingiza sumu nyingi mwilini. Hii hutokana na matumizi ya mbolea zenye kemikali na dawa za kuulia wadudu waharibifu kwenye mazao. Vile vile vyakula vya mifugo kama kuku huwekewa kemikali ambazo sio salama kwa matumizi. Hivyo ni vizri kujitahidi kula mboga, matunda na nyama za kienyeji hili kupunguza kiwango cha sumu zinazoinia kwenye mwili.
Changamoto nyingine ni kupata kiwango sahihi kutokana na mahitaji ya siku. Hivyo basi ni muhimu kutumia Supplements ili kuhakikisha unapata kiwango sahihi cha vitamini hizi na kwenye njia sahihi.
Wasiliana nasi kwa namba +255755518289 kwa maswali na maelezo zaidi juu ya changamoto ya “Hormonal Imbalance”.
Wasiliana na daktari wako kabla ya kutumia virutubisho vyovyote kwa ajili ya “hormonal imbalance” kwa wanawake.

Friday, November 16, 2018

UZITO ULIOKITHIRI



UZITO ULIOKITHIRI
Uzito uliokithiri au Obesity ni changamoto ambayo hutokana na mwili kuhifadhi mafuta kwa wingi. Hii hupelekea mwili kutofanya kazi vizuri na kuongeza uwezekano wa kupata changamoto za kiafya kama presha, kisukari na magonjwa ya moyo.
Habari njema ni kwamba, hata punguzo dogo la uzito linaweza likaboresha au kuzuia changamoto za kiafya ambazo hutokana na kuwa na uzito uliokithiri. Mabadiliko ya milo, kuongeza ufanyaji wa mazoezi na mabadiliko ya tabia yanaweza kusaidia kupunguza uzito. Dawa na upasuaji nazo ni njia zingine za kusaidia mtu kuondokana na changamoto ya uzito uliokithiri.
Dalili
Uzito uliokithiri hupimwa kwa kuangalia uwiano kati ya urefu na uzito au BMI. BMI ikiwa imefika 30 au zaidi basi hapo inasemekana mtu huyo ana uzito uliokithiri. BMI hupimwa kwa kugawanya uzito wako kwenye kilogramu kwa urefu wako kwenye mita na kipeo cha pili.
Kwa watu wengi kipimo hiki hutoa makisio mazuri ya kiwango ya mafuta mwilini. Hata hivyo, kipimo cha BMI hakipimi kiwango cha mafuta kwenye mwili, hivyo kwa watu wengine, kama wanyanyua vyuma wanaweza kuwa na BMI kwenye kundi la watu wenye uzito uliokithiri ingawa hawana mafuta mengi mwilini. NI muhimu kumuuliza daktari wako kama una BMI iliyopitiliza.

Visababishi
Ingawa uzito uliokithiri unaweza kusababishwa na genetiki, tabia na homoni, uzito ulikothiri haswa husababishwa na kula chakula kingingi kuliko mwili unavyohitaji ili kuweza kufanya kazi. Mwili wako huifadhi kile chakula kilichopitiliza kama mafuta.
Vifuatavyo ni visababishi vikuu vya uzito uliokithiri;
·         Kutofanya Mazoezi. 
·         Kula hovyo.
·         Genetiki.
·         Mfumo wa maisha wa familia.
·         Changamoto za kiafya.
·         Baadhi ya dawa. 
·         Changamoto za kijamii na kipato. 
·         Umri. 
·         Ujauzito. 
·         Kutopumzika. 
Hata kama una moja au zaidi ya visababishi hivi haimaanishi kuwa lazima utakuwa na uzito uliokithiri. Unaweza kuhakikisha haupati changamoto ya uzito ulikithiri kwa kuhakikisha unakula mlo kamili, unafanya mazoezi na kubadili tabia ambazo zinakupelekea kunenepa.
Changamoto
Kama una uzito uliokithiri una hatari ya kupata changamoto kubwa za kiafya kama;
·         Kuwa na mafuta mengi kwenye damu
·         Kisukari
·         Presha ya kupanda
·         Metabolic syndrome
·         Magonjwa ya moyo
·         Kiharusi
·         Saratani, zikiwemo saratani ya mfuko wa uzazi, shingo ya kizazi, endometrium, ovari, matiti, utumbo, figo, kongosho, ini na tezi dume.
·         Changamoto ya kupumia.
·         Changamoto za uzai kwa wanawake, kama ugumba na mzunguko mboya wa hedhi.
·         Changamoto za nguvu za kiume na afya ya uzazi kwa wanaume.
·         Changamoto za mifupa na maungio yake.



Ubora wa Maisha
Unavyokuwa na uzito uliokithiri, ubora wa maisha yako kwa ujumla unaathirika. Unaweza ukashindwa kufanya vitu ambavyo ulikuwa unafanya kama kushiriki kwenye shughuli zinazokuletea furaha. Unaweza ukahepuka kwenda kwenye sehemu zenye watu wengi au ukanyanyapaliwa sababu ya uzito wako.
Kuzuia
Kama upo kwneye hatari ya kuwa na uzito uliokithiri, una uzito mkubwa au una uzito ulio sahihi, unaweza kuchukua hatua kuzuia kuongezeka uzito na changamoto za=inazokuja na uzito mkubwa. Haishangazi kuwa hatua za kuchukua ili kuzuia kuongezeka uzito ndio hizo hizo za kuchukua ili kupunguza uzito: mazoezi ya kila siku, mlo kamili, na kudhamiria kuamgalia unachokula na kunywa mwa muda mrefu.
·         Mazoezi. Unahitaji dakika 150 mpaka 300 za mazoezi kwa wiki ili kuzuia kuongezeka uzito. Mazoezi haya ni kama kutembea, kukimbia, kuendesha baiskeli, kuogelea nk.
·         Kula mlo uliokammilika. Kula vyakula vyenye kalori chache na vyenye virutubisho vingi kama matunda, mboga mboga na nafaka ambazo hazijakobolewa. Kaa mbali na vyakula vya mafuta, sukari na pombe. Kula milo mitatu kwa siku na usile sana kati kati ya milo.
·         Vifahamu na vihepuke vishawishi vinavyokufanya ule hovyo. Fahamu ni vitu gani au hali gani ukufanya ule hovyo.
·         Pima uzito wako mara kwa mara. Watu wanaopima uzito wao angalau mara moja kwa wiki wana nafasi kubwa ya kutoongezeka uzito.
·         Kuwa na muendelezo. Kuendelea na mpango wako wa kula kwa kuzingatia afya kati kati ya wiki, mwisho wa wiki na unavyosafiri hukuongezea nafasi ya kuwa na mafanikio zaidi.


Kwa mawasiliano zaidi na kama una maswali juu ya njia za kupunguza uzito unaweza ukawasiliana nasi kwa namba +255 755 518 289.
Bofya HAPA kuchat na mtaalam wa masuala ya uzito na kupunguza uzito.