Vitamini 4 Muhimu
kwa kubalance hormones kwa Wanawake.
Je ni vitamini zipi muhimu kwa ajili ya kuratibu hormones kwa wanawake?
Kutokuwa na uwiano sahihi wa hormone ni chanzo cha changamoto nyingi za kiafya
kwa wanawake.Wanawake hupitia mabadiliko mengi ya hormone kwenye maisha yao –
wakati wa hedhi, PMS, ujauzito na wakati wa kukoma hedhi.
Mabadiliko haya ya hormone yanaweza kusababisha kula hovyo, kukosa
nguvu, msongo wa mawazo, chunusi, na maumivu. Pia yanaweza kusababisha
changamoto ya vimbe kwenye ovary au kwa lfha ya kitaalam, PCOS.
Sababu za “Hormonal Imbalance” kwa
wanawake.
Kuna sbabu nyingi za “hormonal imbalances” kwa wanawake.
Kutokana na mchakato wa asili wa kuzeeka, kutoka kwenye hedhi mpaka
kukoma hedhi, mabadiliko ya hormones hutokea.
Lakini, kuna mambo mengine kwenye mazingira kama uchafuzi wa mazingira,
vyakula vya viwandani, sumu kwenye bidhaa za usafi na urembo, nyama za
viwandani pia hujulikana kwa kuvuruga uwiano wa hormone.
Vyakula navyo vina mchango mkubwa sana kwenye afya na uwiano wa
hormones. Kula vyakula vingi vyenye sukari, mafuta, wanga, vihifadhi vya bandia
(artificial preservatives), na kupuuzia ulaji wa vyakula vyenye vitamini,
madini na viondosha sumu kama matunda, mboga mboga, mafuta mazuri, vyama za
kienyeji (organic) na vyakula jamii ya karanga huunyima mwili virutubisho
muhumi ambavyo hhuitajika kwa ajili ya kuweka uwiano sahihi wa hormones. Kwa
sababu ni vigumu kupata virutubisho vyote muhimu kwa wingi unaohitajika kila
siku, ni muhimu kutumia “Nutritional Supplements”.
Ingawa unahitaji kuwasiliana na daktari wako ili upate vipimo na
matibabu sahihi ya “hormonal imbalance” na matatizo yanayohusiana nayo, unaweza
ukaongeza ulaji wa vitamini hizi kwenye chakula chako. Hizi zitakusaidia
kurekebisha tatizo la “Hormonal Imbalance” kwa njia asilia.
Sasa tunagalie vitamini muhimu kwa ajili ya “Hormonal Imbalances” kwa
wanawake:
Vitamini 4
Muhimu kwa kubalance hormones kwa Wanawake.
1. Vitamini C
Vitamini C ni vitamini namba moja kwenye kuusaidia mwili kutengeneza
hormone ya progesterone. Idadi kubwa ya wanawake wenye umri wa kuzidi miaka 35
hupata changamoto ya kuwa na upungufu wa hormone hii ya progesterone. Upungufu
wa progesterone husababisha msongo wa mawazo, kukosa usingizi, na kuwa na
wasiwasi.
·
Kiwango kinachohitajika: 75 – 100 mg kwa
siku.
·
Matunda yana kiwango kizuri cha Vitamini
C. Unaweza ukala machungwa, machenza, kiwi, strawberries na mananasi
yana kiwango kizuri cha vitamini C.
2. Vitamini D
Wanawake wengi wana changamoto ya upungufu wa vitamini D ingawa ni vitamin
muhimu sana. Upungufu wa vitamini D husababisha maumivu ya viungo, ukosefu wa
nguvu, msongo wa mawazo, changamoto za tezi (thyroid).
·
Kiwango kinachohitajika: 400 – 800 IU
kwa siku.
·
Vyanzo vizuri vya Vitamini D ni pamoja na dakika
20 za jua kila asubuhi, kiini cha yai, uyoga, na samaki.
3. Vitamini B-6
Moja kati ya vitamini muhimu kwenye “hormonal imbalance” kwa wanawake ni
Vitamini B-6. Vitamini B-6 inasaidia kwa kupunguza dalili za PMS kwa wanawake
kama moods, hasira, kusahau sahau, na tumbo kujaa gesi.
·
Kiwango kinachohitajika: 50 – 100 mg kwa
siku.
·
Vyanzo vizuri vya Vitamini B-6 ni kama njegere,
maini ya ng’ombe, samaki na kuku.
4. Vitamini E
Vitamini E ni kiondosha sumu kizuri sana. Ni muhimu kwa kila mwanamke
ambaye anapitia ukomo wa hedhi maana hupata upungufu wa hormone ya “estrogen”. Kupata 50-400 IU kwa siku itasaidia kuratibu "hot flashes", ukavu kwenye uke, na "mood swings" ambavyo vyote hutokana na upungufu wa hormone ya estrogen.
·
Kiwango kinachohitajika: 22.4 IU kwa
siku.
·
Vyanzo vizuri vya Vitamini E ni kama mafuta
ya mimea,maharage, nafaka zisizo kobolewa, na almonds.
Matumizi ya
Supplements
Kutokana na mabadiliko ya
mazingira na njia za kulima mimea na matunda zilivyobadilika, ni rahisi
kuingiza sumu nyingi mwilini. Hii hutokana na matumizi ya mbolea zenye kemikali
na dawa za kuulia wadudu waharibifu kwenye mazao. Vile vile vyakula vya mifugo
kama kuku huwekewa kemikali ambazo sio salama kwa matumizi. Hivyo ni vizri
kujitahidi kula mboga, matunda na nyama za kienyeji hili kupunguza kiwango cha
sumu zinazoinia kwenye mwili.
Changamoto nyingine ni kupata
kiwango sahihi kutokana na mahitaji ya siku. Hivyo basi ni muhimu kutumia
Supplements ili kuhakikisha unapata kiwango sahihi cha vitamini hizi na kwenye
njia sahihi.
Wasiliana nasi kwa namba
+255755518289 kwa maswali na maelezo zaidi juu ya changamoto ya “Hormonal Imbalance”.
Wasiliana na daktari wako kabla ya kutumia virutubisho vyovyote kwa ajili
ya “hormonal imbalance” kwa wanawake.
No comments:
Post a Comment