UZITO ULIOKITHIRI
Uzito uliokithiri au Obesity ni changamoto ambayo hutokana na mwili
kuhifadhi mafuta kwa wingi. Hii hupelekea mwili kutofanya kazi vizuri na
kuongeza uwezekano wa kupata changamoto za kiafya kama presha, kisukari na
magonjwa ya moyo.
Habari njema ni kwamba, hata punguzo dogo la uzito linaweza likaboresha
au kuzuia changamoto za kiafya ambazo hutokana na kuwa na uzito uliokithiri.
Mabadiliko ya milo, kuongeza ufanyaji wa mazoezi na mabadiliko ya tabia
yanaweza kusaidia kupunguza uzito. Dawa na upasuaji nazo ni njia zingine za
kusaidia mtu kuondokana na changamoto ya uzito uliokithiri.
Dalili
Uzito uliokithiri hupimwa kwa kuangalia uwiano kati ya urefu na uzito au
BMI. BMI ikiwa imefika 30 au zaidi basi hapo inasemekana mtu huyo ana uzito
uliokithiri. BMI hupimwa kwa kugawanya uzito wako kwenye kilogramu kwa urefu
wako kwenye mita na kipeo cha pili.
Kwa watu wengi kipimo hiki hutoa makisio mazuri ya kiwango ya mafuta
mwilini. Hata hivyo, kipimo cha BMI hakipimi kiwango cha mafuta kwenye mwili,
hivyo kwa watu wengine, kama wanyanyua vyuma wanaweza kuwa na BMI kwenye kundi
la watu wenye uzito uliokithiri ingawa hawana mafuta mengi mwilini. NI muhimu
kumuuliza daktari wako kama una BMI iliyopitiliza.
Visababishi
Ingawa uzito uliokithiri unaweza kusababishwa na genetiki, tabia na
homoni, uzito ulikothiri haswa husababishwa na kula chakula kingingi kuliko
mwili unavyohitaji ili kuweza kufanya kazi. Mwili wako huifadhi kile chakula
kilichopitiliza kama mafuta.
Vifuatavyo ni visababishi vikuu vya uzito uliokithiri;
·
Kutofanya Mazoezi.
·
Kula hovyo.
·
Genetiki.
·
Mfumo wa maisha wa familia.
·
Changamoto za kiafya.
·
Baadhi ya dawa.
·
Changamoto za kijamii na kipato.
·
Umri.
·
Ujauzito.
·
Kutopumzika.
Hata kama una moja au zaidi ya visababishi hivi haimaanishi kuwa lazima
utakuwa na uzito uliokithiri. Unaweza kuhakikisha haupati changamoto ya uzito
ulikithiri kwa kuhakikisha unakula mlo kamili, unafanya mazoezi na kubadili
tabia ambazo zinakupelekea kunenepa.
Changamoto
Kama una uzito uliokithiri una hatari ya kupata changamoto kubwa za
kiafya kama;
·
Kuwa na mafuta mengi kwenye damu
·
Kisukari
·
Presha ya kupanda
·
Metabolic syndrome
·
Magonjwa ya moyo
·
Kiharusi
·
Saratani, zikiwemo saratani ya mfuko wa uzazi, shingo ya kizazi,
endometrium, ovari, matiti, utumbo, figo, kongosho, ini na tezi dume.
·
Changamoto ya kupumia.
·
Changamoto za uzai kwa wanawake, kama ugumba na mzunguko mboya wa hedhi.
·
Changamoto za nguvu za kiume na afya ya uzazi kwa wanaume.
·
Changamoto za mifupa na maungio yake.
Ubora wa Maisha
Unavyokuwa na uzito uliokithiri, ubora wa maisha yako kwa ujumla
unaathirika. Unaweza ukashindwa kufanya vitu ambavyo ulikuwa unafanya kama
kushiriki kwenye shughuli zinazokuletea furaha. Unaweza ukahepuka kwenda kwenye
sehemu zenye watu wengi au ukanyanyapaliwa sababu ya uzito wako.
Kuzuia
Kama upo kwneye hatari ya kuwa na uzito uliokithiri, una uzito mkubwa au
una uzito ulio sahihi, unaweza kuchukua hatua kuzuia kuongezeka uzito na
changamoto za=inazokuja na uzito mkubwa. Haishangazi kuwa hatua za kuchukua ili
kuzuia kuongezeka uzito ndio hizo hizo za kuchukua ili kupunguza uzito: mazoezi
ya kila siku, mlo kamili, na kudhamiria kuamgalia unachokula na kunywa mwa muda
mrefu.
·
Mazoezi. Unahitaji dakika 150 mpaka 300
za mazoezi kwa wiki ili kuzuia kuongezeka uzito. Mazoezi haya ni kama kutembea,
kukimbia, kuendesha baiskeli, kuogelea nk.
·
Kula mlo uliokammilika. Kula vyakula
vyenye kalori chache na vyenye virutubisho vingi kama matunda, mboga mboga na
nafaka ambazo hazijakobolewa. Kaa mbali na vyakula vya mafuta, sukari na pombe.
Kula milo mitatu kwa siku na usile sana kati kati ya milo.
·
Vifahamu na vihepuke vishawishi vinavyokufanya ule
hovyo. Fahamu ni vitu gani au hali gani ukufanya ule hovyo.
·
Pima uzito wako mara kwa mara. Watu
wanaopima uzito wao angalau mara moja kwa wiki wana nafasi kubwa ya
kutoongezeka uzito.
·
Kuwa na muendelezo. Kuendelea na
mpango wako wa kula kwa kuzingatia afya kati kati ya wiki, mwisho wa wiki na
unavyosafiri hukuongezea nafasi ya kuwa na mafanikio zaidi.
Kwa mawasiliano zaidi na kama una maswali juu ya njia
za kupunguza uzito unaweza ukawasiliana nasi kwa namba +255 755 518 289.
Bofya HAPA kuchat na mtaalam wa masuala ya uzito na kupunguza uzito.
No comments:
Post a Comment