Sunday, November 18, 2018

MAGONJWA YA MOYO



MAGONJWA YA MOYO

Utangulizi
  • Watu million 17.9 hufa kwa magonjwa ya moyo dunia nzima kila mwaka. Huu ni sawa na 31% ya vifo vyote duniani.
  • Zaidi ya 75% ya vifo hivi hutoka kwenye nchi zenye uchumi wa chini na wa kati.
  • 85% ya vifo vyote visababishwavyo na ugonjwa wa moyo husababishwa na mshtuko wa moyo au kiharusi.


Magonjwa ya moyo au cardiovascular diseases ni magonjwa ambayo hutokana na moyo kutofanya kazi vizuri au changamoto kwenye mishipa inayosafirisha damu. Magonjwa haya ni kama, coronary artery disease, changamoto ya  mmapigo ya moyo, kiharusi, maumivu ya kifua (angina) na changamoto za kuzaliwa nazo.

Changamoto nyingi zinazotokana na magonjwa ya moyo zinaweza kuzuiwa au kutatuliwa kwa kufanya mabadiliko kwenye mfumo wa maisha.


Dalili

Dalili za kuwa na magonjwa ya moyo ni;
  • Maumivu ya kifua.
  • Kuishiwa pumzi au kupumua kwa shida.
  • Maumivu, Ganzi, Ulegevu au Ubaridi kwenye miguu au mikono kama mishipa ya damu kwenye hivyo viungo imebana.
  • Maumivu kwenye shingo, taya, kootumbo la juu au mgongo.
  • Mapigo yasiyo na mpangilio maalum.
  • Kuvimba miguu.
  • Uchovu.
  • Kizunguzungu.

Inawezekana usijulikane kuwa una magonjwa ya moyo mpaka ukipata mshtuko wa moyo hivyo ni muhimu kuhakikisha unacheki hizi dalili za magonjwa ya moyo na ujadiliane na daktari wako kama una wasi wasi wa kuwa nayo.




Vitu vinavyoweza kusababisha magonjwa ya moyo
  • Umri. Umri huongeza hatari ya mishipa ya damu kuharibika au kusinyaa na misuli ya moyo kulegea au kutanuka.
  • Jinsia. Wanaume wana hatari kubwa ya kupata magonjwa ya moyo. Ingawa hatari huongezeka kwa wanawake baada ya kukoma hedhi. 
  • Historia ya familia. Historia ya familia ya magonjwa ya moyo huongeza hatari ya kupata magonjwa hayo haswa kama mzazi alipatwa ugonjwa mapema (umri wa miaka 55 kwa ndugu wa kiume, kama baba au kaka, na umri wa 65 kwa ndugu wa kike kama dada au mama). 
  • Uvutaji wa sigara. Nicotine inayopatikana kwenye sigara hufanya mishipa ya damu kuziba na carbon dioxide uharibu kuta za mishipa ya damu na kusababisha changamoto za magonjwa ya moyo. Wavuta sigara hupatwa na mishtuko ya moyo zaidi ya wasiovuta sigara. 
  • Tiba za mionzi kwa wagonjwa wa saratani. Baadhi ya dawa na tiba za mionzi za saratani zinaweza kuongeza hatari ya kupata magonjwa ya moyo. 
  •  Ulaji mbaya. Ulaji wa vyakula vyenye mafuta, sukari, chumvi na lehemu huchangia kwenye kukua kwa magonjwa ya moyo.
  • High blood pressure. Kiwango cha pressure ya damu kikiwa juu sana huweza kusababisha kutanuka kwa kuta za mishipa ya damu na kupunguza uwazi unaopitisha damu.
  • Kisukari. Kuwa na kisukari huongeza hatari ya kupata magonjwa ya moyo.
  • Uzito Uliokithiri. Uzito uliokithiri huongeza changamoto kwa kiasi kikubwa sana.
  • Msongo wa mawazo. Msongo wa mawazo husababisha uharibifu wa mishipa ya damu na kuoneza changamoto.


Kuzuia

Baadhi ya magonjwa ya moyo, kama hitilafu kwenye moyo, hayawezi kuzuilika. Bali unaweza ukazuia magonjwa mengi ya moyo kwa kubadili mfumo wako wa maisha. Mabadiliko hayo ni kama;

·         Kuacha uvutaji wa sigara na kukaa na wavutaji wa sigara.
·         Dhibiti magonjwa mengine kama kisukari, high blood pressure na lehemu.
·         Fanya mazoezi kwa dakika 30 kila siku kwa angalu siku 4 kwa wiki.
·         Kula vyakula visivyo na mafuta mengi na chumvi.
·         Kuwa na uzito sahihi.
·         Punguza msongo wa mawazo.



Tiba

Magonjwa ya moyo yana matibabu tofauti kutokana na changamoto yenyewe. Kwa mfano, kama changamoto ni maambukizi (infection) basi antibiotics zitatumika kuweza kutibu. Kwa ujumla, magonjwa ya moyo hutibiwa kwa hizi njia zifuatazo;
  • Mabadiliko ya tabia. Hii ni pamoja na kula vyakula vyenye mafuta kidogo na chumvi kidogo, kufanya mazoezi angalu kwa dakika 30 kwa siku angalau mara 4 kwa wiki,kuacha uvutaji wa sigara na kunywa pombe kwa kiasi. 
  • Dawa. Kama mabadiliko ya tabia hayatoshelezi, daktari wako atakuandikia dawa kuweza kuratibu ugonjwa wa moyo. Aina ya dawa itatokana na ugonjwa wenyewe. 
  • Upasuaji. Kama dawa nazo hazitoshelezi, daktari wako atashauri upasuaji mdogo/mkubwa ili kurekebisha tatizo.



Hitimisho

Magonjwa mengi ya moyo yanaweza kuhepukika na kurekebishwa kwa kubadilisha mfumo wa maisha. Kwa kupunguza uzito na kufikia uzito sahihi kutokana na urefu wako. Punguzo la kilo 5 linaweza kusaidia kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa ya moyo na mengine yasiyoambukizwa kwa asilimia kubwa. Pia kula milo iliyokamilika isiyokuwa na mafuta mengi na chumvi nyingi. Mazoezi pia husaidia kwenye kuhakikisha moyo unafanya kazi vizuri lakini pia kwenye kupunguza uzito.

Kwa ujumla, unaweza kurekebisha afya yako kwa kubadili mambo madogo madogo kwenye maisha yako.

Kwa maswali zaidi na ushauri wa jinsi unavyoweza kuyazingatia haya kwa njia rahisi wasiliana nasi kwa namba +255 755 518 289.

Karibu sana.





No comments:

Post a Comment